Thursday, 13 April 2017
TCRA yazitoza faini kampuni za simu, Zadaiwa kutozingatia vigezo vya utoaji huduma
Seebait.com 2017SeeBait
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imezipiga faini zaidi ya milioni 65 kampuni tisa za simu nchini kwa kosa la kushindwa kukidhi baadhi ya vigezo vya ubora wa huduma kinyume na matakwa ya kanuni ya 9,10 na 11 ya kanuni za ubora wa huduma za 2011
Akiongea jana na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa TCRA, Mhandisi James Kilaba alizitaja kampuni hizo kuwa Benson Informatics Limited Smart, Airtel Tanzania, Vodacom Tanzania, Zanzibar Telecom Limited Zantel, Mic Tanzania Limited, Tigo, Viettel Tanzania limited, Halotel, na Tanzania Telecommunications Company Limited, TTCL huku akizitaka kampuni hizo kuhakikisha zinatoa huduma bora.
"TCRA inawakumbusha watoa huduma wote wa mawasiliano nchini kuhakikisha mnatoa huduma zinazokidhi ubora wa sauti na upakuaji wa hali ya juu (Kudownload) pamoja na kufuata sheria za huduma ya mawasiliano ya mwaka 2011". Alisema Kilaba
Aidha Mhandisi huyo alisema wataendelea kuwachukulia hatua wale wote watakaoshindwa kukidhi vigezo vya ubora wa huduma kama ilivyo agizwa.
Advertisement
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
http://mdundo.com/a/35071
-
Mgogoro wa CUF Ulivyoibua Mvurugano Katika Uchaguzi wa Wabunge ELA..... Wakati wabunge saba kati ya tisa watakaoiwakilish...
-
VideoMPYA: Mkali Aslay ametuletea hii inaitwa ‘Angekuona’ By Victor Kileo TZA on April 11, 2017 Share Tweet Share Share comments Sta...

No comments:
Post a Comment